Ufunuo wa Yohana 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 16 (Swahili) Revelation 16 (English)

Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi. Ufunuo wa Yohana 16:1

I heard a loud voice out of the temple, saying to the seven angels, "Go and pour out the seven bowls of the wrath of God on the earth!"

Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake. Ufunuo wa Yohana 16:2

The first went, and poured out his bowl into the earth, and it became a harmful and evil sore on the people who had the mark of the beast, and who worshiped his image.

Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa. Ufunuo wa Yohana 16:3

The second angel poured out his bowl into the sea, and it became blood as of a dead man. Every living thing in the sea died.

Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu. Ufunuo wa Yohana 16:4

The third poured out his bowl into the rivers and springs of water, and they became blood.

Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi; Ufunuo wa Yohana 16:5

I heard the angel of the waters saying, "You are righteous, who are and who were, you Holy One, because you have judged these things.

kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili. Ufunuo wa Yohana 16:6

For they poured out the blood of the saints and the prophets, and you have given them blood to drink. They deserve this."

Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako. Ufunuo wa Yohana 16:7

I heard the altar saying, "Yes, Lord God, the Almighty, true and righteous are your judgments."

Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto. Ufunuo wa Yohana 16:8

The fourth poured out his bowl on the sun, and it was given to him to scorch men with fire.

Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu. Ufunuo wa Yohana 16:9

People were scorched with great heat, and people blasphemed the name of God who has the power over these plagues. They didn't repent and give him glory.

Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu, Ufunuo wa Yohana 16:10

The fifth poured out his bowl on the throne of the beast, and his kingdom was darkened. They gnawed their tongues because of the pain,

wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao. Ufunuo wa Yohana 16:11

and they blasphemed the God of heaven because of their pains and their sores. They didn't repent of their works.

Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. Ufunuo wa Yohana 16:12

The sixth poured out his bowl on the great river, the Euphrates. Its water was dried up, that the way might be made ready for the kings that come from the sunrise.

Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Ufunuo wa Yohana 16:13

I saw coming out of the mouth of the dragon, and out of the mouth of the beast, and out of the mouth of the false prophet, three unclean spirits, something like frogs;

Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. Ufunuo wa Yohana 16:14

for they are spirits of demons, performing signs; which go forth to the kings of the whole inhabited earth, to gather them together for the war of that great day of God, the Almighty.

(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.) Ufunuo wa Yohana 16:15

"Behold, I come like a thief. Blessed is he who watches, and keeps his clothes, so that he doesn't walk naked, and they see his shame."

Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni. Ufunuo wa Yohana 16:16

He gathered them together into the place which is called in Hebrew, Megiddo.

Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. Ufunuo wa Yohana 16:17

The seventh poured out his bowl into the air. A loud voice came forth out of the temple of heaven, from the throne, saying, "It is done!"

Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. Ufunuo wa Yohana 16:18

There were lightnings, sounds, and thunders; and there was a great earthquake, such as was not since there were men on the earth, so great an earthquake, so mighty.

Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. Ufunuo wa Yohana 16:19

The great city was divided into three parts, and the cities of the nations fell. Babylon the great was remembered in the sight of God, to give to her the cup of the wine of the fierceness of his wrath.

Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. Ufunuo wa Yohana 16:20

Every island fled away, and the mountains were not found.

Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno. Ufunuo wa Yohana 16:21

Great hailstones, about the weight of a talent,{1 talent is about 34 kilograms or 75 pounds} came down out of the sky on people. People blasphemed God because of the plague of the hail, for this plague is exceedingly severe.